COVID-19: Wizara ya Afya Yatangaza Watu 906,746 Wamepata Chanjo
Watu 906,746 wamechanjwa dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 nchi nzima kulingana na takwimu za hivi punde kutoka kwa Wizara ya Afya. Kati yao 278,642 wana umri wa miaka 58 na zaidi, wahudumu wa afya ni 159,982, walimu 141,571 maafisa wa usalama 76,578 na raia wa kawaida 249,973.